Usaili wa Maisha Plus Dar ni Sept 22 na 23

 

Usaili wa shindano la Maisha Plus unatarajiwa kukamilika jijini Dar es Salaam mwezi huu. Lakini waratibu wa shindano hilo wana habari njema kwa vijana waliopitwa na usaili kwenye mikoa mingine kama walivyoandika kwenye ukurasa wao wa Facebook:

“Kama utakuwa kwa bahati mbaya katika mikoa ambayo tumeshapita mpaka sasa umeshindwa kufika kwenye usahili wa MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2012,labda ni kwasababu ya kuchelewa kupata taarifa,au ulikuwa na majukumu au matatizo basi hujachelewa sana,kama utaweza panda basi tunakukaribisha kwenye usahili wa DAR ambao utafanyika tarehe 22 na 23 mwezi huu na mahali ambapo usahili huo utafanyika tutawafahamisha.”

Maisha Plus ya mwaka huu imedhaminiwa na OXFAM pamoja na NMB