Uchawi wakithiri Rorya, mbunge kupeleka watu kuhubiri injili

Ulishawahi kusikia story kuwa ujaluoni kuna uchawi wa kufa mtu? Well, ni kweli. Huenda Sumbawanga ikawa imebaki jina tu kwa jinsi uchawi ulivyokithiri wilayani Rorya, mkoani Mara sasa hivi.

Kutokana na kuzidi kwa tatizo hilo mbunge wa jimbo la Rorya, Lameck Airo amewahaidi wananchi wa kijiji cha Nyambogo kata ya Kitembe kupeleka wahubiri wa dini mbalimbali kwa gharama zake  kwa ajili ya  kuhubiri injili kufuatia kukithiri kwa vitendo vya kishirikina.

 

Inadaiwa kuwa katika kijiji hicho  watu wamekuwa wakifa katika mazingira ya kutatanisha na wengine kunyofolewa viungo sehemu za siri.

Akiongea kwenye mkutano wa wananchi  wa kijiji cha Nyambogo jana uliohitishwa na diwani wa kata ya Kitembe , Thomas Patrick  Airo amesema  amefikia uaamuzi huo wa kupeleka  wahubiri baada ya kupata malalamiko hayo ya wananchi .

 

Pia kupitia mkutano huo mbunge huyo aliwataka wachawi wote kuachana na vitendo vya kishirikina  kwani kuendelea kufanya hivyo ni kusababisha familia zao kutengwa na jamii hususani watoto ambao ni wanafunzi na hatimaye kuogopwa na wenzao na kutengwa kutokana na uchawi wa wazazi wao.

Septemba 14 wananchi wenye hasira kali walichoma miji 11 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na uchawi na kuwafukuza ambapo watu hao 52 wakiwa na watoto 80 walikimbilia ofisi ya DC wa Rorya Elias Goroi kuomba kuhifadhiwa.

SOURCE: RFA