Tony Parker apewa dau kuwa refa wa pambano la Chris na Drake
Licha ya Chris Brown na Drake kuipuuzia ofa kubwa ya bilionea Aliki David ya dola milioni 5 kila mmoja ili waingie ulingoni kuzichapa, bado tajiri huyo hajakata tamaa.
Akimtumia promoter wa ndondi nchini Marekani Damon Fieldman, sasa ametoa ofa nyingine kwa mchezaji wa mpira wa kikapu Tony Parker aliyekuwepo kwenye ugomvi wa Chris na Drake ili awe refa kwenye pambano lao.
Tony amepewa ofa ya dola laki tano kuliongoza pambano hilo.
Feldman bado ana matarajio kuwa pambano hilo litafanyika mwezi October japo hakuna kati ya Drake ama Brown aliyekubali kushiriki kwenye pambano hilo.
Mapema mwaka huu, Brown alitania kuwa angeingia ulingoni kuzichapa na Drake.
