Tom Hanks amlilia Michael Clarke Duncan

 

Unamkumbuka ‘Dibo’ wa kwenye Friday? Kwa wapenzi wa filamu za Ice Cube, watakuwa wanamfahamu.

Muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Michael Clarke Duncan amefariki dunia jana.

Muigizaji Tom Hanks ameuambia mtandao wa RumorFix kuwa amesikitishwa vibaya na kifo hicho.

Hanks na Duncan waliigiza kwenye filamu ya The Green Mile.

Muigizaji huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 54.

 “I am terribly saddened at the loss of Big Mike. He was the treasure we all discovered on the set of The Green Mile. He was magic. He was a big love of man and his passing leaves us stunned,” alisema Hanks kwenye maelezo yake.