
THT yatimiza miaka 7
Jumba la vipaji Tanzania, (THT) limetimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwake.
THT ilianzishwa mwaka 2006 jijini Dar es Salaam na Ruge Mutahaba wa Clouds FM kwa lengo la kutoa elimu ya muziki, kucheza na sanaa za jukwaani kwa vijana wenye vipaji.
THT imewatambulisha wasanii wengi wakubwa nchini Tanzania wakiwemo Barnaba, Amini, Linah, Mwasiti, Mataruma na wengine.
Kutokana na kuwa na vipaji vingi, wasanii wa THT wamekuwa wakitumiwa kutumbuiza katika matamasha mbalimbali ya kiserikali na ya kawaida ikiwa pamoja na kufanya show nje ya nchi.