Solothang akana kumdiss Wema Sepetu kwenye Miss Tanzania
Rapper wa Tanzania aishie Dublin, Ireland, Msafiri Kondo aka Solothang amekanusha maneno yaliyoenea kuwa alimemdiss Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu.
Katika wimbo huo uitwao Miss Tanzania, Solothang ameandika mashairi yanayomzungumzia mlimbwende wa Tanzania lakini katika lugha ya picha kumaanisha nchi ya Tanzania na jinsi inavyochezewa na watu wachache.
Akiongea na Dj Fetty wa Clouds Fm, Solothang amesema:
“Yeah mimi mwenyewe nilishawahi kusikia utata huo, kuna watu wengi sana wanasema, kwamba wimbo wa Miss Tanzania nimemuimba Wema Sepetu, wimbo wa Miss Tanzania nimemuimba sijui miss Tanzania, yaani wanaufananisha na walimbwende fulani hapo sio, lakini ukweli ni kwamba sina tatizo na Wema Sepetu, sina tatizo na mrembo yeyote hapo Bongo, kwahiyo sina haja ya kumuimba mrembo yeyote.”
Aliongeza “Chochote wanachokifanya ni biashara yao, ni mambo yao na hiyo nyimbo ukiingalia hata verse ya inasema ‘baba yake alikuwa mkoloni kipindi yule miss mwali’, kwanza hapo inamtoa miss yeyote , hakuna miss ambaye baba yake alikuwa mkoloni. Hiyo inadhihirisha kuwa nazungumzia nchi zaidi kuliko mrembo yeyote, na vile vile kuna mstari unaosema ‘anakifua kimebetuka, sio maziwa ni madini’, mamiss wote wana maziwa kifuani, mimi sizungumzii maziwa, nazungumzia madini. Kwa kifupi nazungumzia nchi yangu Tanzania na vitu vizuri vilivyomo, kuna mlima kilimanjaro, kuna gesi ya songosongo vimetajwa na matumizi yake mabaya. Nahisi Tanzania na rasilimali tulizonazo tunastahili kuwa mbele zaidi ya hapo tulipo. Kwahiyo ni nyimbo inayoleta changamoto ya kimaendeleo katika nchi yetu."
