Soggy atamani kufanikiwa kama AY, Sugu na Profesa Jay

 

Rapper mkongwe nchini Tanzania, Anselm Ngaiza aka Soggy Doggy, amesema anajivunia kuona mafanikio ya wenzake wanaofanya muziki na kazi ya utangazaji kama yeye.

Soggy ambaye pamoja na kufanya vizuri sana kwenye muziki wa kizazi kipya nchini kwa nyimbo zilizohit kama Kibanda cha Simu na zingine bado hajafanikiwa inavyostahili.

 

Pamoja na muziki, Soggy pia ni mtangazaji wa Uhuru FM, na pia aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Free Africa na  Triple A FM ya Arusha.

Kupitia Facebook leo ameandika, “Kuna rafiki zangu najivunia mafanikio yao,ipo siku nitafata nyayo zao...Taji Liundi,Edo Kumwembe,Joseph Mbilinyi,Joseph Haule,Juma Mchopanga,Shy-rose Bhanji,Halima Mdee,Vicent Nyerere,Gadi Kalugendo,Steve Kabuye,Fred Fidelis,Juma Kaseja,Ben Kataluga,Hamis Mwinjuma,AY,Caz-T,Paul James Sweya na wengineo.

Kwa sasa rapper huyo yupo jijini Mwanza katika tour ya muziki aliyoandaa na wenza Bwana Misosi na D-Knob.