Rihanna na Chris wafanya mapumziko mafupi pamoja
Kuna tetesi kuwa Rihanna na Chris Brown wanafurahia mapumziko mafupi pamoja.
Kwa mujibu wa mtandao wa HollywoodLife.com Chris anaweza kuwa alimwalika kuwa pamoja weekend hii kabla ya Chris kuanza ziara yake ya Ulaya na Afrika baadaye mwezi huu.
Chris ambaye ataanza ziara yake November 14 anatarajia kurejea Los Angeles leo (05.11.12) kuzindua taasisi yake ya Symphonic Love Foundation.
Staa huyo anatarajiwa kufanya show nchini Afrika Kusini, Uganda na huenda akaja Tanzania pia.
