Rick Ross kupiga show Nigeria mwezi ujao

 

Rapper wa Miami na bosi wa Maybach Music Rick Ross  atadondoka mwezi ujao nchini Nigeria ‘kumsalimia beautiful Onyinye’ na kupiga show kwenye tamasha la Summer Jam Fest 2012.
 
Rick Ross atatumbuiza jijini Lagos, kwenye hoteli ya Eko and Suites, ambapo tamasha hilo litafanyika.
 
Habari hizo zimekuja wiki chache baada ya rapper huyo kushtakiwa na promoter mwingine wa Nigeria kwa kushindwa kuhudhuria kwenye tamasha hilo la mwaka jana kutokana na suala la usalama hafifu nchini humo.
 
Tamasha hilo litafanyika ijumaa ya August 17, 2012.