
Rich Mavoko asema wimbo wake 'Mapenzi' umevuja
Msanii wa Bongo Flava Richie Mavoko amesema wimbo wake uliosambaa kwenye mtandao umevuja na hakupanga kuuachia sasa.
Akizungumza na Dj Choka, Mavoko amesema haelewi ni nani aliyeusambaza bila ruhusa yake.
Hata hivyo amesema kwakuwa tayari umeshasambaa kwenye mtandao anawaomba watu wa radio wasiucheze kwa sasa mpaka pale atakapotoa ruhusa.