Rais Jakaya Kikwete audhuria mazishi ya Sajuki

Miongoni mwa watu walioudhuria mazishi ya marehemu Sajuki katika makaburi ya Kisutu ni pamoja na Mh Rais J. Kikwete. Msanii huyo wa tasnia ya filamu Bongo ameagwa na maelfu ya watu, wakiwemo viongozi mbalimbali serikalini, wadau wa Bongo movie, wadau wa burudani, wapenzi wa burudani na wengine wengi. Mh Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana mbalimbali wakati wa shida na raha nchini na kujitokeza kuungana na wananchi wengine katika mazishi wa wasanii wa kibongo yatokeapo ambao wamekuwa kama kioo cha jamii nchini.

Mungu amlaze mahali pema peponi Sajuki na mchango wake utakumbukwa daima katika tasnia ya filamu nchini.