Picha mpya za Blue Ivy zaleak mtandaoni

 

Picha mpya za mtoto wa Beyonce, Blue Ivy Carter zimevuja tena kupitia mtandao maarufu wa udaku nchini Marekani, MediaTakeOut.com!

Ingawa picha hizo hazionekani vizuri, zinamuonesha mtoto huyo akiwa amebebwa na mama yake kipindi ambacho alikuwa bado hajakua sana.

Mtoto huyo ambaye bado hakujatolewa picha rasmi ili kumwona vizuri alivyo sasa anaonekana kwenye picha hiyo akifurahia muda na mama yake.

Blue Ivy alizaliwa mwezi January mwaka huu na wazazi wake walikataa ofa ya majarida maarufu duniani kuwalipa ili waoneshe picha zake.

Mpaka sasa watu wengi duniani wamekuwa na hamu kubwa ya kuiona vizuri sura ya mtoto huyo ambaye wazazi wake wameendelea kumficha.