Peter Okoye (P-Square) atarajia kupata mtoto wa pili

 

Baada ya kumpoteza mama yake mwezi uliopita, Peter Okoye wa kundi la P-Square anatarajia kuongeza kiumbe kingine hivi karibuni kupunguza machungu hayo.

Kupitia Twitter leo ameandika, “So Happy!!! We are expecting another child!. Thank God for the gift of life."

Habari hiyo njema inatarajia kuongeza familia yake ambayo tayari ina mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cameron atakayetimia miaka minne mwezi ujao.

Mama wa watoto hao anaitwa Lola Omotayo.