Penzi la Justin Bieber na Selena Gomez bado moto

 

Justin Bieber na mpenzi wake Selena Gomez hawajapigwa picha wakiwa pamoja kwa muda sasa lakini kutokana na ripoti zilizoenea wiki iliyopita kuwa uhusiano wao upo matatani wameamua kuthibitisha tofauti.

Selena, 19, alitweet picha ya pamoja na mpenzi wake huyo wakiwa jijini Toykyo, Japan juzi.

 

Wapenzi hao wadogo kiumri ambao wamekuwa kwenye uhusiano wa wazi kwa miezi 16, wameonesha dalili za kuwa amani bado kwenye picha waliyopiga mbele ya ukuta wa rangi na michoro.

"Hi Japan," aliandika kuambatanisha na picha hiyo. "I heart you."

Mrembo huyo amemsindikiza Bieber, 18, kwenye show zake za nje ya nchi.

Bieber pia alishare picha ye performance ya Japan,na alitweet kabla ya show, "Great day exploring in Tokyo. Ready to go hard tomorrow."

Aliongezxa "This is what it's all about. About to perform for my Japanese fans. The love here has been incredible!"