Pancho Latino aajiri bodyguard wa kumlinda?
Hii ni direct message kwa haters kutoka kwa miongoni mwa ‘dopest producers’ in Tanzania, Pancho Latino wa B’Hits. Inaonekana haters wake wamekuwa wengi mno mpaka kuamua kuajiri bodyguard wake.
Jana producer huyo kupitia Facebook aliweka picha akiwa amekaa sehemu, busy na simu yake ya mkononi na kuweka maelezo, “somewhere relaxin with ma bodyguard.”
Pembeni yake anaonekana pande la mtu ambaye tunahisi hucheka kwa nadra sana akiwa makini kumlinda bosi wake.
Ama ni swagga tu hizi? Yaani huenda alikuwa ameenda klabu na kumuomba bodyguard wa klabu hiyo wapige picha ili kuosha Facebook?

Seriously Pancho, kuna umuhimu wa kuwa na bodyguard Tanzania hii ambayo amani imejaa tele? Anyways, kama ni kweli tunaheshimu uamuzi huo kwakuwa mfuko wako unaruhusu kufanya hivyo ama kama kuna watu wanatishia maisha yako. Sounds like B’Hits inalipa!!
