P-Funk amdiss Marco Chali kwenye Twitter?
Producer wa mkongwe wa Tanzania anayeaminika kuwa na mchango mkubwa wa kuupa heshima muziki wa Bongo Flava, P-Funk Majani jana ameandika kitu kwenye mtandao wa Twitter kinachoonekana kama ni diss kwa Marco Chali.
Hiyo ni baada ya Majani kumwandikia Master J tweet kuwa angependa kufanya naye kazi kwenye project yake na Karabani na sio Marco Chali.
“Bro wea working on a serious album, karabani and I. We would luv to have u bless us with a track!! Not Marco but u,” alitweet Majani na Master Jay kujibu, “Noted, I’ll give u a call in a bit.
Baada ya muda Majani alitweet tena, “EATV/Radio askin me why I dissed Marco, I didn't Diss Marco, I respect his work. But want the sound of the legend MJ!!”
Mwisho Master Jay alitweet, “Eh! Just an honest misunderstanding though.”
