Octopizzo aisema siri ya mafanikio yake

 

Katika mamc wenye uandishi mkali nchini Kenya kwa sasa huwezi kuacha kumtaja Octopizzo. Ni rapper anayeheshimika licha ya kupata umaarufu hivi karibuni tu. Utajiri wake umewafanya baadhi ya wakenya kuanza kudai kuwa amejiunga na Illuminati.

Hata hivyo rapper huyo aliyekulia kwenye mazingira duni ya Kibera amesema mafanikio yake yamekuja kwa kuhusstle na sio uiIlluminati.

Akiongea na kipindi cha Citizen Radio cha Mambo Mseto jana, Octo aliweka wazi kuwa alikuwa amejiweka ahadi kuwa angeacha muziki kama usingempa maisha lakini muziki umempa kile anachostahili.

“Illuminati haiezi andikia ma artiste lyrics, ni bidii yako inadetermine your rise to fame,” alisema.

“Kueni waoga ju am unpredictable! Mi si ka weather. More is yet to come.”