Nokia 1100 ndio simu iliyouzika zaidi duniani!!
Wakati ambapo soko la simu limefurika simu za kila aina, ni bora kufahamu simu gani iliyowahi kuuzika zaidi duniani ambao si nyingine zaidi ya Nokia 1100. Huenda wewe ni miongoni mwa watu waliowahi kuimiliki simu hii.
Zaidi ya simu milioni 200 za aina hiyo ya simu zimeuzwa duniani tangu zitoke 2003, na kufanya kuwa simu zilizouzwa zaidi ama kifaa cha electronic kilichouzika sana. Kwa sasa Nokia haitengenezi tena simu za aina hiyo.
Simu hizo zilitengenezwa kuzilenga nchi zinazoendelea duniani na kwa watumiaji ambao hawahitaji mambo mengi zaidi ya kupiga, kupokea simu na meseji.
