Nisher: Video ya Belle 9 ikitoka itazua mjadala

Director wa video anayekuja kwa kasi nchini, Nisher amesema video ya Belle 9 ambayo ameidirect itazua mjadala ikitoka,

Tayari blog na website kadhaa za Bongo zimeanza kuizungumzia video hiyo itakayotoka mwakani.

“Binafsi Nmefurahia sana Kazi yangu!!! Belle9 Ni Msanii Makini sana na nimeupenda Moyo wake sanaaaaa... amenisikiliza kwa makini sana wakati wa Filming na ku-Act!! Actually ni Actor Mzuri sana,  waliendana sana na Actress Mwenzake Lizz !! OK ngoja nisiongee sana...ntatuma zaidi baadae, video inatoka January 2013.