Nikki Mbishi apuuzia wazo la kufanya club banger

 

Wazo la kufanya club banger bado halijapata nafasi kwenye akili ya Nikki Mbishi aka Baba Malcom ambaye ameendelea kusimamia misingi anayoiamini ya Hippop hata kama muziki hautampa chochote.

Mbishi amejipatia umaarufu nchini kwa conscious hip hop na zile watu wa Arusha wanaziita NGUMU NYEUSI.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni ushauri kutoka shabiki, Nikki ameshauriwa kutembelea Kenya na kufanya ngoma moja ya club, wazo ambalo hata hivyo ameonesha kulipuuzia kwa kicheko.

“I think u should also visit kenya kisha mtafute HOMEBOYZ PRODUCTION for some club bangers.nairobians lav club songs,mfano kama ile ngoma u collabod wit stereo,one na ben pol.3 club bangers in Nairobi will make ya filthy rich hehehe...” ameyaweka maneno hayo ambayo ametumia na mtu kwenye inbox ya Facebook.