Ndege ya Precision Air yapata ajali Kigoma (Hakuna majeruhi)
Ndege ya shirika la Precision Air nchini Tanzania imepata ajali leo (July 24) mkoani Kigoma wakati ikitua.
Tukio hilo limesababishwa na matairi kupasuka wakati ndege hiyo ilipokuwa inatua kwenye uwanja wa ndege.
Shirika hilo limethibitisha tukio hilo kupitia mtandao wa Twitter.
"We would like to confirm that one of our aircraft had an incident in Kigoma this afternoon when tyres burst after landing. No injuries."
