Muonekano mpya wa Daz Baba!! Azikata rasta zake
Anaweza kuwa amepotea kwa muda mrefu kwenye muziki wa Tanzania lakini bado yupo na anaendelea kuhangaika na muziki. Hivi karibuni aliunda kundi lenye members watatu liitwalo Tanzaniano ambalo hata hivyo halikufanya vizuri.
Good news ni kuwa hivi karibuni atasikika tena kwenye airwaves za radio mbalimbali nchini. Producer mkongwe nchini Tanzania wa Bongo Records, P-Funk Majani ameamua kumrudisha tena kwenye ramani.
Na huu ndio muonekano mpya wa member huyo wa kundi lililotamba sana la Daz Nundaz ambapo ameamua kukata rasta zake. Unauonaje muonekano wake mpya?
