Mume wa Goldie adai ndoa yao ilibaki kuwa ya siri kutokana na kazi yake

Andrew Harvey, mume wa Uingereza wa marehemu Goldie, amesema hakuwa na tatizo na jinsi mke wake alivyokuwa akiishi na kudai kuwa yeye pia alimshauri awe controversial  kwasababu ni nzuri kwa biashara ya burudani.

Alipouliwa kama alikubaliana na vitendo vya Goldie alipokuwa kwenye jumba la BBA, alisema: Sisi (Goldie na mimi) tulijua  ugumu wa show hiyo na tulijua mikakati ya mchezo. Nadhani alifanya vizuri sana, nilisema fanya vitu controversial  sababu watu wanapenda.’”

Kwenye mahojiano na Punch Andrew, ambaye ni engineer, alidai kuwa ndoa yao na Goldie ilikuwa ya furaha na hivi karibuni walipanga kuwa na watoto. Alisema aliamua kuwa kimya muda wote sababu ya uhalisia wa kazi yake.

“Goldie and I preferred this way (secrecy) because I did not want media attention because of my work. I had no disagreement with her lifestyle and I encouraged her to follow her dreams. We often joked about being together like a pair of old slippers,” alisema.

“I did not want her to say ‘if only’ when we were wearing those slippers. That was why I encouraged her to live her dreams.”

Andrew pia alikanusha ripoti kuwa mke wake alikuwa akitumia madawa ya kulevya.