Mshindi wa Nokia Don’t Break the Beat kupewa mkataba wa kurekodi na Decimal Media/Universal Records

 

Mshindi wa kwanza kwenye shindano la Nokia Asha Don’t Break atakula shavu la kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Decimal Media/Universal Records pamoja na kitita cha shilingi milioni tano za Tanzania.

Mkataba huo utamfanya mshindi arekodi nyimbo na kufanya video tatu katika kipindi cha mwaka mmoja huku kwenye video moja akifanya collabo na rapper wa kike Stella Mwangi, STL.

Akiongelea mkataba huo mkurugenzi mtendaji wa Decimal Records Eric Musyoka, amesema anayo furaha kufanya kazi na vipaji vipya vya Afrika Mashariki kupitia shindano hilo la Nokia.

Tangu mwezi uliopita msako wa kumpata mkali wa michano Afrika Mashariki umeendelea kwa kuzunguka kwenye miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu, Eldoret, Kampala na Dar-es-Salaam.

Mashindano hayo yameingia kwenye raundi ya pili ambapo yatahusisha battle za kwenye klabu katika miji kadhaa ya Kenya, Kampala na Dar-es-Salaam ambako wasanii wawili watachaguliwa. 

Watakaoperform kwenye show hizo ni pamoja na STL, Octopizzo, Maddtraxx na Mwana FA.

Fainali ya Afrika Mashariki itafanyika mapema September ambapo wachanaji 12 watapambana kuwapata wasanii wawili katika hao atapatikana mshindi.