Mpoki aachia ngoma mpya – Mademu

 

Mchekeshaji wa kundi la Original Comedy Mpoki, leo ameachia ngoma mpya iitwayo Mademu.

Ngoma hiyo aliyomshirikisha mwanamuziki wa THT Barnaba, imetayarishwa na producer Lamar wa Fishcrub Audio Station.

Katika track hiyo Mpoki amezungumzia utofauti uliopo kati mademu wa uswahili na wale wanaoishi kwenye familia bora.

Akiongea na Clouds Fm leo, Mpoki amesema kwa mfano ukiangalia suala la elimu utagundua kuna utofauti mkubwa wa course wanazochagua wasichana walio kwenye familia bora na wale wanaotoka kwenye familia maskini.

Amesema wasichana waliozaliwa kwenye familia bora huchagua kusoma course za gharama kama za ‘Air Ticketing’ na zingine ambazo ada yake ni kubwa wakati wale maskini huishia kusoma kozi kama za ualimu kwakuwa ndizo wanazomudu kuzilipia.

Mpoki amesema utofauti huo ndio unaoleta matabaka makubwa kati ya wale walionazo na wasiokuwa nazo.

Ameongeza kuwa japokuwa katika nyimbo zake hutumia maneno ya utani, lakini lengo lake ni kuufikisha ujumbe kwa serikali ili ikumbuke kuwajibika zaidi kuwajali wananchi wake wanaoishi maisha magumu.