
Mfahamu mbongo anayemiliki Lamboughini!
Kwa mashabiki wa Yanga jina la Davies Mosha si geni! Aliwahi kuwa makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo. Lakini upande mwingine wa maisha yake unaweza usiwe unajulikana sana! Jamaa anamiliki kitu cha Lamboughini. Miongoni mwa gari zenye gharama kabisa duniani!
\Thamani yake kwa madafu, yaani hela ya Tanzania ni kama bilioni moja hivi!
Gari lake lina rangi ya njano na kwa kulimiliki gari hili anaingia kwenye orodha ya watu wenye magari yenye thamani zaidi barani Africa.
Akizungumza na gazeti la Championi Ijumaa Mosha amesema gari hilo ni la matumizi yake na familia na kula bata tu! Hana mengi!
Gari hili amelinunua kwa mtoto wa Bakhresa (Yusuph), Julai 2011.
Akizungumzia kero anazozipata kwa kuwa na gari hilo amesema “Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.
Source: GLOBAL PUBLISHER