May D: Sina taarifa kama nimefukuzwa P-Square Records

 

Muimbaji wa Nigeria aliyeipendezesha ngoma ya P-square, Chop My Money, May D amesema hana taarifa kuwa amepigwa chini kwenye label ya Square Records kama ilivyotangazwa juzi.

Amesema aliamka tu na kukutana na taarifa hizo kuwa hayupo tena kwenye label hiyo.

Maelezo yaliyokuwa yana sahihi ya Square Records siku ya jumanne yalisema kuwa msanii huyo wa kwanza kusainishwa kwenye label hiyo hawako naye tena.

Sababu za ni kutokana na tofauti zisizosuluhusika.

May D alisainishwa na Square Records miezi kadhaa iliyopita.

Alikuwepo kwenye mazishi ya mama yao Peter na Paul, Mrs Okoye,August 2, 2012 katika jimbo la Anambra.