Martin Kadinda aendelea kupata mashavu nje ya nchi

 

Wiki chache zilizopita, mbunifu wa mavazi anayekuja juu nchini Tanzania, Martin Kadinda, alipata shavu la kufanyiwa mahojiano na kituo ch M-NET baada ya kukubali kazi zake. 

Nyota yake imeendelea kung’ara kimataifa baada ya kupata shavu lingine nchini Marekani.

“Kwa mara ya Kwanza Maishani mwangu nitakanyaga Ardhi ya marekani Ijumaa hii, nitakuwa the only Designer Mwalikwa katika Africa New York fashion...... Kivumbi collection itaonekana tena ndani ya New York.. kivumbi collection Hiyoooo.. single button hizooo and Ofcourse Vibunduki teheheteetehehehhe,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kadinda amejipatia umaarufu nchini Tanzania baada ya nguo zake za Single Button kufanya vizuri na ambazo zimevaliwa na wasanii wengi wa Bongo Flava wakiwemo Diamond, Hemed na Ommy Dimpoz.