Marc Anthony asaini kuwa mwalimu kwenye The 'X Factor'.

 

Mwanamuziki mkongwe Marc Anthony amesaini mkataba wa kuwa mwalimu kwenye shindano la The 'X Factor'.

Mshindi huyo wa Grammy na mwandishi wa nyimbo atakuwa akifanya kazi na Simon Cowell kwenye talent show hiyo kumsaidia kuchukua wasanii wazuri kwenye kipengele chake.

Habari hizi zimekuja siku chache tu baada ya Justin Bieber naye kutajwa kuwa mwalimu kwenye show hiyo inayotarajia kuanza kuruka September 12 kupitia kituo cha Fox.