Mama yake Ray C asema dawa za matibabu kwa mwanae ni ghali, anahitaji msaada

Mama yake mzazi na msanii wa kike nchini Rehema Chalamila aka Ray C amesema binti yake yupo kwenye matibabu baada ya kuathirika vibaya na matumizi ya madawa ya kulevya lakini dawa anazotumia ni aghali hivyo anahitaji msaada kwa wasamiria wema.

Mama huyo aitwaye Margret Mtweve amesema amekuwa akipewa ushauri wa aina mbalimbali ambao mwisho wa siku umekuwa wa maneno zaidi usio na msaada mkubwa wakiwemo wale wanaosema apelekwe kwa mganga wa kienyeji. Ameongeza kuwa mpaka sasa bado hajapata msaada wa maana.

Ameongea kuwa muda yuko na mwanae akihangaika naye licha ya baadhi ya watu kumtumia meseji kuwa amemtelekeza mwanae.

Ameitaja namba yake kuwa ni 0655999700 na kuwataka waumini wamuombee Ray C.