
Madee aikubali ngoma mpya ya Dogo Janja
Mara nyingi hating is unhealthy and showing love hata kwa watu waliokuzingua is always vice versa na pia unapata baraka kutoka mbinguni!
Wengi walitegemea Madee ataichukia ngoma mpya ya Dogo Janja ‘Ya Moyoni’ kwa kuhisi kuwa amezungumzwa yeye lakini haijawa hivyo.
Akizungumza na East Africa Radio leo, Madee amekiambia kipindi cha Powers Jams kuwa bado ni shabiki mkubwa wa dogo huyo na ameikubali ngoma yake mpya.
Anasema amependa zaidi chorus iliyofanywa na PNC lakini ameongeza kuwa kama angeisikia kabla ya kupelekwa redioni angependekeza yafanyike marekebisho kadhaa.
Miezi kadhaa iliyopita Madee na Dogo Janja walikuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya Tanzania baada ya Madee kushutumiwa kumtumia kiuchumi msanii huyo kiasi cha kufanya aondoke Tip Top Connections.
Kwa sasa Dogo Janja yupo chini ya kampuni ya Mtanashati Entertainment.