Lil Wayne alazimika kutua nusu ya safari ya ndege baada ya kupatwa dalili za kifafa

Rapper wa YCMCB Lil Wayne amelazimika kutua katikati ya safari yake jimboni Texas  baada ya kupatwa na dalili kama za kifafa akiwa kwenye private jet.

Chanzo kilicho karibu na Weezy ambaye jina lake ni Dwayne Michael Carter, Jr kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa rapper huyo alipelekwa hospitali jana mchana (saa za Marekani) kwaajili ya kupata matibabu.

Inadaiwa kuwa Wayne alikaa hospitali kwa masaa kadhaa.

Haijulikani kama madaktari wamegundua alichosumbuliwa lakini sasa anaendelea vizuri.