Lauryn Hill aitosa Interview ya Oprah Winfrey!

 

Ni ngumu kuamini kuwa malkia wa show za mazunguzo duniani Oprah Winfrey, ametoswa na staa kwaajili ya interview lakini hicho ndicho kilichotokea baada ya Lauryn Hill kukataa kushiriki kwenye kipindi cha Oprah's Next Chapter.

Baada ya kufanya interview iliyofanikiwa weekend iliyopita na Rihanna, Oprah yupo mbioni kufanya interview na mshindi wa medali ya dhahabu kwenye Olympic iliyopita Gabby Douglas, weekend ijayo.

Hata hivyo sehemu ambayo amegonga mwamba ni kwa muimbaji wa 'Doo Wop (That Thing)'  Lauryn Hill.

Baada ya shabiki mmoja kumuuliza Oprah kuhusu kumtafuta Lauryn kwa interview, Oprah alijibu: "Tried. She said no."

Pengine Lauryn hataki kuonekana sana mbele ya umma kwakuwa anasubiria hukumu yake ya kukwepa kulipa kodi pamoja na nia ya watu kutaka kujua masuala ya baba wa mtoto wake aliyezaliwa mwaka jana.