Lady Jaydee kuifungua Diary yake Jumapili hii

Jumapili hii mwanamuziki na mjasiriamali wa kike nchini Tanzania, Judith Mbimbo aka Lady Jaydee anatarajiwa kuizundua rasmi reality TV show yake aliyoipa jina la Diary ya Lady Jaydee. Uzinduzi huo utafanyika kwenye kiota chake cha Nyumbani Lounge ambapo bendi yake ya Machozi itakuwa ikitumbuiza na kuwapa raha wageni waalikwa.

Diary ya Lady Jaydee itakuwa ikioneshwa kupitia kituo cha runinga cha East Africa Television. Show hiyo itakuwa ikimuonesha msanii huyo mwenye mafanikio makubwa katika maisha ya kawaida akiwa kama mke wa mtu, mjasiriliamali, mwanamuziki n.k.