
Kevin Hart asema atamfunga kamba Kanye West ili asivamie stage ya VMA kama mwaka 2009
MC wa MTV Video Music Awards Kevin Hart ametania kuwa atamfunga Kanye West kamba kwenye kiti chake ili kumzuia asivamie tena kwenye stage ya tuzo hizo kama alivyofanya mwaka 2009.
Katika tuzo za VMA mwaka 2009, rapper huyo alimkatiza mwanamuziki Taylor Swift aliyekuwa akitoa skurani baada ya kushinda tuzo ya Best Female Video, na Kanye kusisitiza kuwa mshindi alitakuwa kuwa Beyonce.
Mchekeshaji huyo amesema hawezi kukubali mwaka huu Kanye afanye tena kituko hicho.
''What we did this year was we banned the artists who could embarrass themselves."
''With Kanye we’ve got a seatbelt for his seat that he can’t get out of, little things that they never thought of in the past to make sure it all goes ok this year,''alisema Hart.
MTV VMA zitafanyika Los Angeles Staples Center kesho September 6.