
Kenya na Tanzania zamwokoa Prezzo
Tanzania na Kenya ni nchi pekee zilizomwokoa Prezzo na panga la eviction jana.
Kenya ambako ndiko Prezzo anatokea, imempigia kura zaidi mtu wao ili kuendelea kumwekea uhakika wa kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa na hatimaye kujihakikishia kurudi nyumbani na kitita cha dola laki 3.
Kama historia inavyosema kwamba mama yake Prezzo ni mtanzania, basi hilo linajidhihirisha kwa watanzania kuwa mstari wa mbele kumpigia kura pia.
Urafiki alionao na wasanii wengine wa Tanzania hususan Ay na MwanaFa umemsaidia kwakuwa wasanii hao wamekuwa mstari wa mbele kuwasisitiza watanzania kumpigia kura Prezzo.
"Kenya really appreciates the effort and help you and your fellow country peeps put in voting for Prezzo to stay in the BBA house," ni tweet ya wakenya iliyoelekezwa leo na wakenya.
Jana mshiriki mwingine kutoka Kenya, Malonza na Junia kutoka Namibia waliyaaga mashindano hayo.
Hivi ndivyo Afrika ilivyopiga kura na kuamua matokeo ya jana.
Angola: Junia
Botswana: Lady May
Ghana: Goldie
Kenya: Prezzo
Liberia: *Goldie / Lady May
Malawi: Kyle
Namibia: Lady May
Nigeria: Goldie
South Africa: Lady May
Sierra Leone: Lady May
Tanzania: Prezzo
Uganda: Kyle
Zambia: Malonza
Zimbabwe: Lady May