Karrueche Tran amcheka Rihanna baada ya interview na Oprah Winfrey

 

Baada ya interview ilivyojichukulia umaarufu ya Rihanna na Oprah Winfrey, mpenzi wa sasa wa Chris Brown amedaiwa kumkejeli Rihanna.

Katika interview hiyo iliyorushwa juzi usiku, Rihanna aliamua kuweka wazi jinsi anavyoendelea kumpenda mpenzi wake huyo wa zamani na kwamba ataendelea kumpenda.

Hata hivyo mpenzi mpya wa Chris Karrueche Tran ameoneshwa kutofurahiswa na maneno ya adui yake huyo ambaye alitumia muda mwingi kumzungumzia mpenzi wake.

Baada ya saa chache tangu kuruka kwa interview hiyo Karrueche alitumia Twitter kuonesha alivyojisikia.

Hata hivyo hakutaka kuandika maneno mengi bali kwa ufupi kabisa aliandika tu kicheko "Lol."

Mashabiki wake waliamua kumuuliza kama kicheko hicho kimetokana na interview hiyo japo aliwapotezea.