Kanye West kupiga show Afrika Kusini Feb 2
Rapper wa Marekani Kanye West anatarajiwa kupiga show nchini Afrika Kusini tarehe 2 mwezi February, 2013.
Mshindi huyo wa tuzo kibao atapiga show moja tu mjini Johannesburg.Tiketi za kuingia kwenye show hiyo zinauzwa kuanzia R650 hadi R1,000.
Rapper wa Afrika Kusini HHP amepangwa kama msanii wa nyumbani atakayemsindikiza Yeezy.
HHP aka Hip-Hop Pantsula amethibitisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa kuandika: , “Bona, I’m proud to announce that yours truly, (Jabba Man) will be performing at the Kanye West concert on the 2nd of February. Ayeye! Haosa tlale, wa dutla.”
