
Julio wa BBA kuzindua wimbo wake mpya Ijumaa hii
Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa Stargame 2012, Julio ameingia rasmi kwenye muziki na Ijumaa hii atazindua wimbo wake wa kwanza.
Wimbo huo uitwao The Nigerian na ambao amemshirkisha Baby utazinduliwa kwenye kiota SYNERGY LOUNGE Oysterbay jijini Dar es Salaam katika party ya Facebook.
Katika party hiyo pia kutakuwa na Dance Performance ua "Tridashanz huku madj wakali Dj Steve B/Skills,Dj Bike ma Dj Dave wakiwasha moto.