JCB afunga ndoa na mchumba wake Diana Jørgensen
Rapper wa Watengwa, JCB Makalla amefunga ndoa rasmi na mchumba wake Diana Jørgensen waliyezaa naye mtoto mmoja. Ndoa hiyo inayoonekana kuwa ya serikali imefanyika jijini Arusha wanakoishi na kuhudhuriwa na ndugu na jamaa zao wa karibu.