JB & KING MAJUTO

 

MWIGIZAJI mahiri na mtayarishaji katika tasnia ya filamu za kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefanya kweli baada ya kuingiza sokoni kazi yake mpya iitwayo ‘Nakwenda kwa Mwanangu’, akimshirikisha gwiji, Amri Athuman ‘King Majuto’.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam juzi, JB alisema kuwa, anaamini filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Jerusalem, itakuwa moto wa kuotea mbali, kwani imelenga kuwaelimisha na kuwaburudisha wananchi.
Aliwataka wananchi, kutoikosa filamu hiyo aliyodai kuwa, mtu anapoiangalia, anaweza kushindwa kuamini kama ni filamu, badala yake kudhani ni matukio ya kweli kutokana na wahusika wote kujitahidi kuvaa uhalisia. “Kwa kweli tunapenda kuwasihi Watanzania, kutoikosa filamu yetu mpya iitwayo ‘Nakwenda kwa Mwanangu’, ndani ya filamu hii kuna ujumbe mzito na miongoni mwa walioshiriki ni King Majuto na mimi'' Kazi kwenu sasa wapenzi wa Bongo moview, kamata copy yako fasta bila kuchelewa!!

Third part source: John Kitime/Tanzania Daima.//JanB Multimedia