Jaguar: I feel bad for Prezzo

 

Msanii wa Kenya wa hit ya Kigeugeu, Jaguar ni miongoni mwa wakenya walioumizwa na kitendo cha Prezzo kukosa ushindi wa Big Brother Afrika uliomwendea Keagan wa Afrika Kusini.

Jaguar ambaye alikuwa akimpigia debe Prezzo kwenye mitandao ya jamii ameliambia gazeti la The Star kuwa hata yeye alikuwa akimpigia kura Prezzo. "Nilitaka sana Prezzo ashinde. Najisikia vibaya kuwa hajapoteza tu miezi minne kwenye BBA bali pia hakuzipata hela. Hata hivyo hajapoteza yote, anaweza kurudi na kuendelea kufanya muziki na hata kuanza kuigiza.”

Pamoja na Prezzo kukosa ushindi huo, nyota ya msanii huyo imeendelea kung’aa baada ya kutangazwa kama balozi maarufu wa One Campaign, shirika linalofanya kampeni ya kutokomeza umaskini na maradhi duniani.

Akiwa balozi wa shirika hilo, Prezzo atahudhuria na kuperform kwenye concert ya Jay-Z baadaye mwezi huu.