Hussein Machozi kushare stage moja na Wyre na Juacali

 

Msanii wa Bongo Flava, Hussein Machozi ameendelea kukubalika zaidi nchini Kenya ambapo kesho atapanda stage moja na wasanii wa ‘List A’ wa Kenya wakiwemo Wyre na Juacali.

Show hiyo itafanyika jijini Nairobi kwenye ukumbi wa KICC ambapo kutakuwa na shindano la MR & MISS JKUAT.

Wakali wengine watakaopanda ni  mwanadada AVRIL, OCTOPIZZO  na RABBIT!

Ni muda mrefu Hussein amekuwa akiutumia nchini Kenya kiasi cha kuwa na wazo la kupafanya makazi yake ya kudumu.

Msanii huyo anakubalika zaidi nchini humo kuliko ilivyo Tanzania.