
Hatimaye Drake ahitimu high school
Rapper wa YMCMB Drake hatimaye amehitimu high school ikiwa ni miaka kumi baada ya kuacha.
Rapper huyo mwenye miaka 25 kutoka Canada hatimaye jana amepata diploma ikiwa ni baada ya miezi kadhaa ya kujisomea kwa bidii.
Msanii huyo wa 'Take Care' alionesha furaha yake kupitia Twitter na kushare habari njema kwa mashabiki wake.
Aliandika: "97% on my final exam. 88% in the course. One of the greatest feelings in my entire life. As of tonight I have graduated high school! "Thank you to my teacher Kim Janzen for spending the last 5 months working tirelessly with me!! OVO SOUND."
Drake aliacha kuendelea na shule akiwa na miaka 15 ili kutafuta maisha kwa kuigiza tamthilia maarufu nchini Canada iitwayo 'Degrassi: The Next Generation'.