Hakuna mtanzania aliyemo kwenye Afribiz charts!!

Imetushangaza kidogo tulipogundua kuwa hakuna hata wimbo mmoja wa msanii wa Tanzania aliyepo kwenye  chart ya Afribiz! 

Wengi watakuwa hawazifahamu hizi chart lakini zina heshima kubwa na zinachukuliwa kama charts za billboard za Africa!

Kinachotusikitisha ni kuwa katika nyimbo hamsini hakuna msanii wa Bongo hata mmoja aliyeingia kwenye chart.

Wakenya na waganda walau wamo. 

Pia waganda wana haki ya kujisifia kwakuwa wiki hii Keko ndo amekamata nafasi ya kwanza kwenye chart hii na wimbo wake Make you Dance.

Labda tujiulize tu ina maana hakuna msanii wa Tanzania aliye na vigezo vinavyohitajika kuingia kwenye chart hizo?

Mpaka AY, MwanaFA na Diamond wameitwa kuperform BBA maana yake ni kuwa muziki wa Bongo unatambulika na waafrika wengine pia!

Soma vigezo hivi na ujiulize kama hakuna msanii aliyevifikia, na kama wapo basi kuna tatizo sehemu!

1.   Radio & TV airplay

2.   Record sales

3.   Radio & TV charts (Top 10’s & Top 20’s etc.)

4.   You Tube views

5.   Electronic & Print media appearances

6.   Artists who reside in the continent of Africa.

7.   Artists with albums not older than a year.

8.   Artists with albums, mixtapes & singles.

9.Artists who will meet the high standards of quality e.g Videos, album packaging (Sleeves), sales indications, You tube views etc..