Fid Q adai beat ya Danger iliibiwa na mmarekani na si yeye aliyecopy
Wiki hii wachekeshaji wa kundi maarufu la Orijino Komedi walimshutumu Fid Q kuwa alicopy na kupaste beat ya wimbo wake Danger.
Hata hivyo kutokana na maelezo ya Fid kundi hilo ndilo lililochemka kwa kutokuwa na uhakika wa kile lililochokisema.
Akiongea na Dj Fetty wa Clouds Fm weekend hii, rapper huyo amesema beat ya Danger alitumiwa na producer aitwaye Choba wa Marekani ambaye yeye na msanii wa huko, J-Brynt walipenda kazi ya Fid Q iitwayo I am Professional na kuamua kumtumia beat hiyo.
Kuhusu namna alivyoipata beat msanii huyo mwingine Fid alisema:
“Huyu msanii mwingine alijaribu kuongea na Choba atumie ile kwaajili ya mixtape akawa amevuka mipaka akataka kufanya mpaka video kitu ambacho kilisababisha ashindwe kuilipia na akaingia mitini na ndio maana ni msanii ambaye hapatikani Twitter, Facebook wala hana website naweza kusema kwa namna moja ama nyingine kuwa huyo jamaa ni mwizi, sio mimi niliyeiba bali mimi na Chomba ama chofaco records ndio tumeibiwa ile beat.”
