D’Banj kuwapeleka Big Sean na Pusha T nchini Nigeria

Msanii nguli wa nchini Nigeria, D’Banj amepanga kuwapeleka wasanii wenzie wa lebo ya GOOD Music nchini Nigeria kumpa shavu kwenye show yake ya sikukuu ya Christmas.

D'banj atafanya show hiyo kwenye ukumbi wa Expo kwenye hoteli ya Eko Hotel and Suites jijini Lagos akiwa na wasanii wenzie wa G.O.O.D Music  Big Sean na Pusha T.

Hata hivyo bosi wake Kanye West hatoweza kwenda kwenye show hiyo ingawa muigizaji Idris Elba anadaiwa kuwa atahudhuria.