
David Guetta afunga ndoa tena baada ya miaka 20 ‘ndoani’
Mtayarishaji wa muziki na DJ maarufu duniani David Guetta na mkewe Cathy wametimiza miaka 20 tangu waoane na jana waliamua kukumbushia ahadi zao za ndoa mbele ya ndugu na watu wao wa karibu.
Sherehe hiyo imefanyika kwenye kisiwa cha Ibiza, Hispania.
Producer huyo mwenye umri wa miaka 44 aliyefanya kazi na wasanii wakubwa duniani ana watoto wawili hadi sasa, Tim, 8, na Angie,5.
Mke wake Cathy ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na meneja wa klabu moja ya usiku.