Darecha 2012 Business Ideas Competition
Katika pitapita yetu mtandaoni tumekutana na hii kitu. Sasa kama wadau wa maendeleo ya kijamii tumeona tuitupie kwenye page zetu ili Watanzania waichangamkie. Darecha 2012 Buiness Ideas Competition; Shindano hili litajumuisha vijana wenye ari ya ujasiriamali walio na umri kati ya miaka 16-25. Washiriki watashindana kwa kuwasilisha MAWAZO yao ya kibiashara. Washiriki watakaofanya vizuri watachaguliwa kuingia katika hatua ya fainali. Washiriki hao bora watapata nafasi ya kuwasilisha michanganuo yao kwa jopo la majaji litakalojumuisha: wafanyabiashara, wakufunzi wa biashara vyuoni na wataalamu wa masuala ya kibenki.
Washiriki watakaoingia fainali watahudhuria mafunzo ya ujasiriamali, watapewa vyeti vya ushiriki na watapata nafasi ya kufahamiana na wajasiriamali waliofanikiwa katika biashara zao. Watapata pia nafasi ya kufahamiana na kuunganishwa na watu na taasisi zinazoweza kuwasaidia kifedha, kimafunzo na kiushauri(mentorship) jinsi ya kujenga miradi yao.Washiriki wote wa hatua ya fainali watainigia kwenye mtandao mkubwa wa vijana wajasiriamali wa Darecha. Washindi watatu wa kwanza watapatiwa zawadi nono.
MUHIMU:1.Uongozi wa Darecha unaahidi kulinda na kutunza mawazo yako utakayowalisha.Tunatambua wewe ndiye mmiliki halali wa mawazo yako. 2.Kujionea mafanikio ya miaka ya nyuma (2009,2010 na 2011) tembelea www.darecha.org
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao.
SIMU: +255714576917 AU +2550654578886
EMAIL: applications@darecha.org
Jinsi ya kuomba tembelea website yao: https://www.darecha.org/
All the best wadau//JanB Multimedia
