Cyrill: Jina la mixtape halimaanishi mimi Freemason

 

Rapper Cyrill Francisco aka Kamikaze, amekanusha uvumi ulioanza kuenea mtandaoni kuwa yeye ni Freemason baada ya kuachia mixtape yenye jina la The Devil’s Boy (Mtoto wa Shetani).

Amesema hilo ni jina tu na halina uhusiano wowote na maana hiyo.

Akiongea na Clouds Fm leo, Kamikaze amesema ameamua kuichia mixtape hiyo online pekee kwa kuwa anaamini kuwa mashabiki wake wanaweza kukaa nayo kwa muda mrefu.

Katika mixtape hiyo, Cyrill amefanya ngoma na maproducer wapya zaidi akiwemo Samtimber wa jijini Arusha ambapo amemshirikisha Lavosti.